Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Akagua Vyanzo vya Maji Dodoma, Aagiza Mradi wa Farkwa Uanze Haraka

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA), Mhandisi David Pallangyo (kushoto) kuhusu mfumo wa kutoa maji safi kwenye chanzo cha maji cha Mzakwe hadi kwenye matangi makubwa yaliyoko jijini Dodoma wakati alipokagua mitambo ya maji safi katika Kituo hicho jijini Dodoma, Novemba 21, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Mwandishi wetu- PMO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) na Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma wahakikishe mradi wa bwawa la maji Farkwa uliopo kijiji cha Mombose, wilayani Chemba, mkoani Dodoma unaanza mapema.

Akizungumza wakati alipotembelea eneo la mradi huo leo (Jumamosi, Novemba 21, 2020) Waziri Mkuu amesema idadi ya watu katika mkoa wa Dodoma imekuwa ikiongezeka kwa kasi hivyo ni lazima kuwepo na chanzo cha maji cha uhakika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *