Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi wa Mji wa Serikali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma ramani ya Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi wa mji huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mipango Miji katika jiji la Dodoma, William Alfayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Kulia ni Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe kuhusu Ujenzi wa Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa jengo Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya kusuka nondo kwa ajili ya nguzo za jengo la Ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Msingi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

28 thoughts on “Waziri Mkuu Akagua Ujenzi wa Mji wa Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *