Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Akagua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa JNHPP

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115 na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka asimamie mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Vilevile, Waziri Mkuu amemwagiza mkandarasi anayejenga mradi huo aukamilishe kwa wakati kwa sababu imebainika kuwa mvua zinazoendelea kunyesha nchini haziathiri utekelezaji wa ujenzi huo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2020) akiwa katika ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo. Amesema ameridhishwa maedeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, kazi inayofanyika ni ya uhakika huku kukiwa na matumaini makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa.”

Mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unajengwa na kampuni ya Arab Construction kwa pamoja na kampuni ya Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye grid ya Taifa na kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Mbali na kuliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kupungua kwa changamoto ya ajira baada ya Watanzania wengi wakiwemo wakandarasi kupata ajira za kudumu na za muda mfupi.

Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya kisasa.

Hafla ya utiaji saini ya Mkataba wa Ujenzi wa Mradi ilifanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Desemba, 2018 na kushuhudiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly. Mradi huu ni njia sahihi ya kufikia Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA,                      

ALHAMISI, MEI 14, 2020.

6 thoughts on “Waziri Mkuu Akagua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa JNHPP

 • August 11, 2020 at 11:15 pm
  Permalink

  I have been browsing online more than three hours today,
  yet I never found any interesting article like yours.
  It is pretty worth enough for me. In my view, if all website owners
  and bloggers made good content as you did, the
  net will be a lot more useful than ever before.
  adreamoftrains best web hosting sites

  Reply
 • August 25, 2020 at 1:07 pm
  Permalink

  Hello, i think that i noticed you visited my weblog so i got here to go back
  the desire?.I’m trying to to find issues to enhance my site!I suppose
  its adequate to use a few of your ideas!! y2yxvvfw cheap
  flights

  Reply
 • August 31, 2020 at 7:30 pm
  Permalink

  Greetings! I’ve been reading your website for a while now and finally got the courage to go ahead and give you a shout out from Houston Texas!
  Just wanted to mention keep up the excellent job!

  Reply
 • September 5, 2020 at 4:36 am
  Permalink

  This is a very good tip particularly to those new to the blogosphere.
  Simple but very accurate information… Many thanks
  for sharing this one. A must read post!

  Reply
 • September 5, 2020 at 9:01 am
  Permalink

  Hey this is kind of of off topic but I was wondering if blogs use WYSIWYG editors or if you have to manually code with HTML.

  I’m starting a blog soon but have no coding know-how
  so I wanted to get advice from someone with experience.
  Any help would be greatly appreciated!

  Reply
 • September 5, 2020 at 12:59 pm
  Permalink

  A motivating discussion is definitely worth comment.
  I believe that you need to publish more on this issue, it may
  not be a taboo matter but usually people do not
  talk about these subjects. To the next! All the best!!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *