Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Aipongeza TPSF kwa Kutoa Ujuzi na Ajira kwa Vijana

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kutoa ujuzi hususani kwa vijana ambao wamewawezesha kujiajiri na kuajiriwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 27, 2021) katika kikao chake na viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na baadhi ya Mawaziri na Watendaji wa Serikali katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema sekta binafsi ndio injini ya maendeleo, hivyo Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi hiyo kwa sababu inaitegemea sana katika kuhakikisha Taifa linasonga mbele kiuchumi.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kufanya maboresho ya sera, sheria na miongozo kwa ajili ya kuiwesha sekta hiyo kutekeleza majukumu yake kama ilivyokusudiwa kwa lengo la kuwa  na uchumi imara.

One thought on “Waziri Mkuu Aipongeza TPSF kwa Kutoa Ujuzi na Ajira kwa Vijana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama