Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Afungua Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Mkoani Ruvuma

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, akiangalia na vikundi vya ngoma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Mbinga Coffee Curing Company, kabla ya kufungua maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amebeba mkaa wa mawe, wakati akikagua mabanda kwenye banda la TANCOAL, katika maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na kulia ni Mkuu wa Jiolojia TANCOAL.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mkaa wa mawe, uliyotengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na wajasiriamali wa kikundi cha Mbalawala Women Group, wakati akikagua mabanda kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kulia ni Meneja wa Fedha wa kikundi hicho, Esta Silas na Msimamizi wa Mradi, Hajra Yakub.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma. Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje John Ndumbalo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

34 thoughts on “Waziri Mkuu Afungua Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Mkoani Ruvuma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama