Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkenda Atua Bandari ya Dar es Salaam, Aendelea na Mkakati wa Kudhibiti Ongezeko la Bei ya Mbolea

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es Salaam

Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amewasili nchini akitokea nchini Morocco ambapo pamoja na mambo mengine katika ziara yake hiyo aliitembelea kampuni ya uuzaji wa mbolea ya OCP ili kuendelea na mkakati wa serikali katika kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa wingi nchini.

Akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam Julai 20, 2021, Waziri Mkenda amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mkakati wa kuhakikisha inadhibiti ongezeko la bei ya mbolea.

Amesema kuwa bei ya mbolea kwenye soko la Dunia imepanda kwa kiasi kikubwa hivyo Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa bei ya mbolea nchini inaendelea kuwa katika ustahimilivu wa bei huku juhudi zikiendelea za kuhakikisha bei ya mbolea inashuka bei.

12 thoughts on “Waziri Mkenda Atua Bandari ya Dar es Salaam, Aendelea na Mkakati wa Kudhibiti Ongezeko la Bei ya Mbolea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama