Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mhagama Kufungua Kikao cha Msajili na Viongozi wa Vyama vya Siasa Kujadili Taarifa ya CAG

Waziri wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama. (Picha kutoka Maktaba)

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenister Mhagama anatarajiwa kufungua kikao cha siku mbili baina ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na viongozi wa kitaifa wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Abuu Kimario, kikao hicho cha Msajili na viongozi wa vyama vya siasa kitafanyika tarehe 29 na 30 ya mwezi huu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa mbili asubuhi na kitawahusu viongozi wa kisiasa na watendaji waandamizi wa vyama hivyo.

Siku ya kwanza ya kikao hicho kitawashusu Wenyeviti wa taifa, Makatibu Wakuu na maafisa wanaohusika na masuala ya kisheria. Siku ya pili itawahusu Wenyeviti Bodi ya Wadhamini, Maafisa Masuuli, wahasibu au weka hazina.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ajenda kuu za mkutano huo ni kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika mwezi Machi mwaka huu.

Mbali na ajenda hizo kuu mbili, taarifa hiyo imeeleza kuwa mada zingine ambazo zinalenga kuondoa migogoro na kuongeza ufanisi kwenye uendeshaji wa vyama vya siasa zitawasilishwa.

Baadhi ya mada zitakazowasilishwa ni pamoja na maadili ya viongozi wa umma, umuhimu wa bima ya afya, jinsi ya kuandaa taarifa za fedha kwa ajili ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wajibu wa bodi ya wadhamini ya chama cha siasa na Sheria ya Vyama vya Siasa kuhusu usimamizi wa mapato na matumizi na vyama vya siasa.

Kikao hicho cha siku mbili baina ya Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi wa vyama vya siasa ni mwendelezo wa juhudi za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhakikisha vyama vya siasa vinajiendesha kama taasisi na kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikiathiri demokrasia ya vyama vingi nchini.

524 thoughts on “Waziri Mhagama Kufungua Kikao cha Msajili na Viongozi wa Vyama vya Siasa Kujadili Taarifa ya CAG

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama