Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Kigwangalla apokea Tuzo Iliyoshinda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Jenerali Mstaafu George Waitara akikabidhi tuzo iliyotolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya TGT jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Jenerali  Mstaafu wa Jeshi, George
Waitara leo amekabidhi kwa Waziri wa Utalii na Maliasili  Dkt. Hamisi Kigwangalla tuzo iliyoshinda
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kutangazwa hifadhi bora barani Afrika.
Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA)
Juni Mosi nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za
kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao,wanyama walao
nyama  na uwepo wa ukanda mrefu wenye
wanyama wengi, tuzo hiyo imepangwa kukabidhiwa kwa Rais Dkt John Magufuli .

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea tuzo iliyotolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hafla iliyofanyika viwanja vya TGT yalipofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf
Mkenda amesema tuzo hiyo imepatikana baada ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
kushindanishwa na Hifadhi nyingine kubwa tano barani Afrika kwa watalii kupiga
kura.Baadhi ya Makamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia tukio hilo katika viwanja vya TGT jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla hiyo sababu za Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupata tuzo hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu, George Waitara akizungumza katika hafla hiyo.
Wawakilishi wa Benki ya NMB pia wameshiriki  katika hafla hiyo.
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akikabidhi tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Jenerali Mstaafu, George Waitara ili aikabidhi kwa Waziri, Dkt. Hamisi Kigwangalla 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Jenerali Mstaafu, George Waitara  akikabidhi tuzo iliyotolewa kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla fupi iliyofanyika  katika viwanja vya TGT jijini Arusha.  
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa
Waziri Kigwangalla, hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGT yanapofanyika
maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA, George Waitara amesema ushindi
wa Hifadhi ya Serengeti kuwa Hifadhi Bora ni ushindi wa Watanzania wote.
 

 

  

FacebooktwittermailFacebooktwittermail