Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Kamwelwe Awasilisha Bajeti ya Trilioni 4.9

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bunge leo Jijini Dodoma.

Kutoka kushoto ni Naibu wa Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Naibu wa Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Elias Kwandikwa wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (katikati) wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mkoani Mwanza, Mhe. Charles Kitwanga wakati wa Kikao cha 24 cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akiteta jambo na Manaibu Waziri wake mara baada ya kumalisha kuwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 Bunge leo Jijini Dodoma. Kutoa kulia ni Naibu Waziri anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Elias Kwandikwa na Naibu Waziri anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Mhadisi Atashasta Nditiye. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

22 thoughts on “Waziri Kamwelwe Awasilisha Bajeti ya Trilioni 4.9

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama