Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Hasunga Azindua Mfumo wa Kuwaunganisha Wakulima na Wanunuzi wa Mazao

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, Leo tarehe 18  Mei 2020. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma 

Ili kukabiliana na uhaba wa masoko ya mazao ya kilimo serikali amezindua mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) ili kuwaunganisha wakulima na wanunuzi wa mazao yatokanayo na Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema kuwa sehemu ya kwanza ni ya huduma za ugani ambayo itamsaidia mkulima kupata huduma na ushauri wa kitaalamu kupitia simu yake ya kiganjani pasipo lazima ya kukutana na Afisa Ugani.

Amesema kuwa huduma hiyo imelenga kutatua changamoto ya idadi ndogo ya Maafisa Ugani hapa nchini ambayo imesababisha wakulima wengi kutokupata huduma za ugani.

Waziri Hasunga ameeleza kuwa sehemu ya pili ni ya huduma za masoko ambayo itamwezesha mkulima kupata taarifa za masoko ikiwemo bei na mahali yalipo masoko kwa wakati husika.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, Leo tarehe 18  Mei 2020. Wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba

Sehemu ya wataalamu mbalimbali wakifuatilia mkutano wa  kazi wa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizindua mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, Leo tarehe 18  Mei 2020.

Vilevile utamwezesha muuzaji kutangaza mazao yake sokoni, mfumo huo pia utawawezesha wakulima na wataalam wa kilimo kuwasiliana kwa kutuma ujumbe kwa njia ya simu za viganjani.

Waziri Hasunga amesema kuwa Mfumo huo umetayarishwa na wizara ya kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Halmashauri husika pamoja na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Jamii -ESRF.

Ameeleza kuwa mfumo huo utafanyiwa majaribio kuanzia tarehe 19 Mei, 2020 katika Wilaya za Bahi, Kongwa na Chamwino kwa muda wa wiki moja.

Katika majaribio hayo, jumla ya Maofisa Ugani 35 na Wakulima 45 kutoka katika kata mbili za wilaya hizo watapata mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huu ambapo Washiriki watapata mafunzo yatakayowawezesha kuwafundisha wengine katika maeneo yao (TOT).

Baada ya majaribio kufanikiwa, mfumo huo utapelekwa kwa wakulima wote nchini kwa ajili ya kuwawezesha kupata huduma za ugani.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, Leo tarehe 18  Mei 2020

Amesema kuwa ili kuweza kupata huduma kupitia M- kilimo mkulima anahitaji kulipia gharama ya ujumbe mfupi (sms) kwa kila huduma atakayohitaji ambapo Katika kipindi hiki cha majaribio (Piloting) gharama zitatolewa na Wizara.

Mfumo huo una faida nyingi, lakini kubwa zaidi ni kufikisha huduma za ugani na za masoko kwa wakulima na wafanya biashara hata wakati wa majanga ya milipuko ya magojwa kama gonjwa la sasa hivi la COVID-19.

Aidha, kutokana na hali ya mlipuko wa ugonjwa wa CORONA, Wizara imejipanga kutekeleza zoezi hilo kwa kuzingatia tahadhali zote muhimu zinazotolewa na wataalam  wa afya pamoja na viongozi nchini.

Waziri Hasunga pia ameeleza kuwa ili kuhakikisha kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani na soko la bidhaa unaleta tija kwa wananchi serikali imeamua kuanzisha aina mbili za masoko ambazo ni soko la awali na soko la upili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akifuatilia mkutano wa kazi wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, Leo tarehe 18  Mei 2020.

Ili kufanikisha utekelezaji wa mifumo hiyo ni lazima kuwepo kwa  vyama hai vya ushirika wa mazao (AMCOS) vilivyo sajiliwa kwa mujibu wa sheria; Kuwepo kwa maghala yaliyosajiliwa; kuainisha aina Mazao yanayohifadhika na kulinda ubora wake; na Elimu ya mfumo kutolewa kwa wananchi.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa M-Kilimo ni kutekeleza maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  aliyeaiagiza wananchi kuwa na uwezo wa kusafirisha mazao kadri wawezavyo bila kulipa kodi kwa mazao ambayo ni chini ya Tani 1 pamoja na Kupunguza usumbufu kwa wakulima.
 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) amesisitiza umuhimu wa soko la awali huku akiwaonya wakulima nchini kutochanganya mazao yao na uchafu ili kuongeza ukubwa wa mzigo.
 
MWISHO

3 thoughts on “Waziri Hasunga Azindua Mfumo wa Kuwaunganisha Wakulima na Wanunuzi wa Mazao

 • March 27, 2021 at 1:56 am
  Permalink

  Thanks a bunch for sharing this with all of us you actually recognize what you are speaking approximately!
  Bookmarked. Kindly also discuss with my web
  site =). We can have a hyperlink alternate
  arrangement among us

  Reply
 • March 28, 2021 at 9:35 am
  Permalink

  Hmm is anyone else having problems with the pictures on this blog loading?
  I’m trying to figure out if its a problem on my end or
  if it’s the blog. Any feedback would be greatly appreciated.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama