Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Dkt. Mahiga Atembelea Banda la TIB ‘Group’

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga akikaribishwa katika Banda la Benki ya TIB na Bw. Daud Masele (kulia) wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametembelea Banda la TIB ‘Group’ linalojumuisha taasisi za Benki ya Maendeleo TIB, Benki ya Biashara ya TIB ‘Corporate’ na Dawati la Huduma za Bima wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Banda hilo alipata fursa za kujionea shughuli za uwekezaji zilizofanywa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mnamo mwaka 1970.

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Benki ya TIB.

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB kutoka kwa Meneja wa Utafiti wa benki hiyo, Dkt. Hildebrand Shayo (kulia) wakati alipotembelea Banda la Benki ya TIB ‘Group’ wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga akiangalia historia na mchango wa Benki ya Maendeleo TIB tangu ilipoanzishwa mwaka 1970.

Akizungumzia nafasi ya taasisi za kifesha katika ukuzaji wa uchumi wa nchi na kuijenga Tanzania ya Viwanda, Balozi Dkt. Mahiga alisema mabenki hasa ya maendeleo kama TIB yana nafasi kubwa katika kutekeleza mipango ya serikali ya kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutoa mikopo ya muda mrefu yenye kuchochea maendeleo katika kukuza biashara,kuongeza ajira, kuwezesha uanzishwaji wa viwanda.

Balozi Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya uwepo wa Benki ya Maendeleo ya TIB ili kuweza kupata mikopo na misaada ya kitaalamu katika uendeshaji wa miradi yao.

49 thoughts on “Waziri Dkt. Mahiga Atembelea Banda la TIB ‘Group’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama