Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Bashungwa Atoa Siku Tano Wakuu wa Mikoa Kuwasilisha Taarifa za Ujenzi wa Madarasa 15,000

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakuu wa Mikoa nchini kuwasilisha taarifa za ujenzi wa vyumba vya madarasa 15,000 kabla au ifikapo Januari 25, 2021.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Januari 20, 2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) linalofanyika kwa siku mbili mkoani humo likiwa na jumla ya Wajumbe 68.

“Natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa kujiridhisha na taarifa hizo kwa kupitia taratibu na miongozo iliyotolewa na kuangalia kama thamani ya fedha katika ujenzi wa vyumba vya madarasa hayo imepatika”, alisema Waziri Bashungwa.

Amesema kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha ari ya kuboresha elimu ya awali, msingi na sekondari nchini kwani katika kipindi cha muda mfupi amewezesha ujenzi wa madarasa 15,000 yakiwemo madarasa 12,000 ya shule za sekondari na madarasa 3,000 kwa ajili ya vituo Shikizi vya shule za msingi hali itakayosaidia kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi.

73 thoughts on “Waziri Bashungwa Atoa Siku Tano Wakuu wa Mikoa Kuwasilisha Taarifa za Ujenzi wa Madarasa 15,000

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama