Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi Wizara ya Utamaduni Wahimizwa Kufanya Kazi Kwa Bidii

Na Shamimu Nyaki  – WUSM, DODOMA

Watumishi  wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wamehimizwa kufanya kazi kwa bidii na kulinda amani,  utamaduni wa mtanzania na kudumisha uzalendo kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Bibi. Zahra Guga, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 23, 2022 Jijini Dodoma.

“Tufanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, Wizara yetu ni miongoni mwa wizara ambazo Sekta zake zinachangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa kupitia ajira za wadau wake”, alisema Bi. Zahra.

Ameongeza kuwa  wizara hiyo ni  nguvu shawishi ya nchi katika kukuza uchumi hivyo watumishi wanapaswa kuzingatia hilo katika utendaji wao kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo kwa kufuata Kanuni, miongozi na taratibu za Serikali, huku wakijielekeza katika kushawishi na kutenda mazuri nje ya maeneo ya kazi.

39 thoughts on “Watumishi Wizara ya Utamaduni Wahimizwa Kufanya Kazi Kwa Bidii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama