Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi NAOT Waaswa Kuzingatia Maadili

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akisisitiza umuhimu wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao , ameyasema hayo wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

Na: Mwandishi Wetu

Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Wameaswa Kuziungatia Maadili wakati wote Wanapotekeleza majukumu yao ili kuendana na dhamira ya Serikali kufikia maendeleo endelevu na uchumi wa kati.

Akizungumza wakati akizindua Baraza jipya la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael amesema watumishi wote wa Ofisi hiyo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia sharia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija katika majukumu wanayotekeleza.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisisitiza umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi wakati wa hafla ya kufungua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akikata utepe kuzindua mkataba wa huduma kwa wateja wakati wa hafla ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

“ Sitarajii Wakaguzi wetu Wakawa miongoni mwa watumishi watakaokumbwa na kashfa za namna yoyote hivyo niwaase kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu,kudai na kupokea rushwa” Alisisitiza Dkt. Michael

Akifafanua amesema kuwa hatma ya makosa hayo ni kupoteza ajira na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama ili sharia iweze kuchukua mkondo wake hali inayoweza kupelekea mhusika kufungwa jela.

Aidha, aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kutumia fursa za Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kujiletea maendeleo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ardhi.

Naibu mkaguzi wa NAOT ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Bi Wendy Masoy akitoa neno la shukrani baada hafla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akisisitiza jambo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad leo Jijini Dodoma baada ya kuzindua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo.

Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa baraza hilo leo Jijini Dodoma.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akiteta jambo na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Mwenwejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michaelwakati wa hafla ya kufungua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) mara baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali Prof. Mussa Assad amesema kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwake ikiwemo kuhakikisha kuwa ripoti ya ukaguzi inatolewa kama inavyotakiwa kila ifikapo mwezi machi.

Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii nyakati zote hali inayoonesha jinsi wanavyojitoa katika kuhakikisha kuwa kazi za ofisi hiyo zinafanyika kama inavyotakiwa.

Baraza la wafanyakazi wa NAOT linafanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili likiwa na dhamira ya kuwaleta pamoja wajumbe kutoka katika Idara, Vitengo, Kada, baadhi ya Taasisi na vyama vya wafanyakazi likiwa ni Baraza la mwaka 2018/2019.

(Picha zote na Frank Mvungi)

 

13 thoughts on “Watumishi NAOT Waaswa Kuzingatia Maadili

 • August 20, 2020 at 2:50 pm
  Permalink

  Where do you come from? methotrexate injection dose for ra Despite her ongoing struggles with weakness and headaches, Maria de Villota was cleared to drive again in February this year, and repeated her intention to continue working with the FIA as part of their Women in Motorsport initiative, aimed at recruiting more female drivers at a professional level. The last woman to enter into the F1 Grand Championship was the Italian Giovanna Amati in 1992, who failed to qualify during three consecutive races in South Africa, Mexico and Brazil, and was eventually replaced by the British future world champion Damon Hill.

  Reply
 • August 20, 2020 at 4:17 pm
  Permalink

  Can I call you back? buy cytotec pfizer The three lead banks had been expected to fund the full termloan if failing to meet demand for the financing before theanticipated closing of the buyout on October 10. However, asmarket sentiment improved this week the lead banks re-launchedthe deal to a wider set of investors at the aforementionedterms, according to sources.

  Reply
 • August 20, 2020 at 5:43 pm
  Permalink

  Punk not dead tamsulosin online uk No wonder offensive coordinator Kevin Gilbride called it a a “challenge.” He added “It’s going to be difficult, but I’m sure those guys are going to give it their best shot and we’ll see what we can do.”

  Reply
 • August 20, 2020 at 6:12 pm
  Permalink

  Go travelling where can i buy levitra online Woodson said Felton would not play against the Raptors, but added that “everybody’s got to go on this trip, yes,” including Bargnani and Stoudemire, who had Sunday off after resuming contact drills the previous day.

  Reply
 • July 12, 2021 at 6:59 pm
  Permalink

  Appreciating the time and effort you put into your blog and in depth information you provide.
  It’s nice to come across a blog every once
  in a while that isn’t the same unwanted rehashed material.
  Excellent read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds
  to my Google account.

  Reply
 • July 26, 2021 at 7:59 pm
  Permalink

  My brother suggested I might like this website. He was entirely right.
  This post truly made my day. You cann’t imagine just how much time I had spent for this info!
  Thanks!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama