Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi 44 wa Sekta ya Ujenzi Kushiriki Miradi Mikubwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga (kushoto) akikabidhi hadidu za rejea za mafunzo kwa Mhandisi Gladiness Kitaly kutoka katika Sekta hiyo ambazo zitamsaidia katika mafunzo yake kwa vitendo kazini katika miradi ya ujenzi wa miundombinu inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Sekta ya Ujenzi imefanikisha zoezi la kuwapeleka watumishi 44 kushiriki mafunzo kwa vitendo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watalaamu kutoka katika Wizara hiyo na taasisi zake ili wawe mahiri katika eneo la Ushauri, Ujenzi na Usimamizi wa miradi mikubwa 11 ikiwemo ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege na mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, wakati akifungua kikao kazi cha mafunzo kwa vitendo kazini ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kwa watumishi hao kujifunza kwa manufaa ya Sekta ya Ujenzi na Taifa kwa ujumla ili kujenga uchumi wa viwanda na hivyo kufanikisha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Wote tunafahamu kuwa hivi sasa ni takribani miaka zaidi ya 50 tokea tupate uhuru lakini miradi mingi inaendelea kutekelezwa na wageni hivyo basi mtumie fursa hii mliyopewa kuwa mabalozi wazuri ili nchi iweze kutengenezamakandarasi na washauri elekezi wazawa wengi miaka ya baadae”, amesisitiza Mwakalinga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga (mwenye suti ya bluu) pamoja na wataalam 44 kutoka katika Wizara hiyo na taasisi zake watakaoshiriki mafunzo yake kwa vitendo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Aidha, amewataka watumishi hao kuwa na nidhamu wakiwa katika maeneo yao ya mafunzo na kutokuwa wajuaji bali waongeze ujuzi kwa yale wanayoyajua na kujifunza kwa bidii teknolojia mpya ambazo walikuwa hawazitumii. Amefafanua kuwa mpango huo utafanyika kwa kipindi cha miezi sita sita na nimoja kati ya mipango ya Wizara iliyojiwekea katika kuhakikisha inaleta chachu yamaendeleo ya nchi hasa katika suala zima la usimamizi na ujenzi wa miundombinu bora.

Arch. Mwakalinga ameeleza kuwa watumishi hao watasaini makubaliano kati yayao na Mwajiri (on job training bond agreement) na pia kupatiwa vitendea kazimuhimu ili kuwawezesha kujifunza kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mtaalam wa Utafiti kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Arch. Neema Fuime, amesema mafunzo hayo ya watumishi kwa vitendo wakiwa kazini itasaidia fedha nyingi zinazotolewa kwenda kwa makandarasiwageni kubaki hapa nchini na thamani ya fedha kuonekana kwa kuwa wasimamizina washauri watakuwa ni wazawa wenye uchungu wa nchi yao.

Naye Mkadiriaji Majengo kutoka Bodi ya Usajili na wakadiriaji Majenzi (AQRB)Joseph Ringo, ameishukuru Serikali kupitia Wizara kwa kutoa fursa hiyo kwawatumishi na kumuahidi Katibu Mkuu huyo kushirikiana kikamilifu na wataalamhao na ameahidi kutoinagusha Serikali iliyowaamini katika na kuwapeleka kwenyemiradi mikubwa ya kitaifa katika suala la usimamizi, ujenzi na ushauri.

Watumishi hao 44 wamepelekwa mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Dar esSalaam, Morogoro, Njombe, Ruvuma na Mtwara ambapo miradi mikubwa ya miundominu inayoendelea kutekelezwa.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail