Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watoa Huduma za Mawasiliano Wapewa onyo Kuvujisha Taarifa Binafsi za Wateja

Na Faraja Mpina -WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe, Dkt. Faustine Ndugulile ametoa onyo kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kuacha tabia ya kuvujisha taarifa binafsi za wateja kwa kuwadhibiti baadhi ya watumishi wao wasio waaminifu.

Ndugulile amebainisha hayo wakati akizungumza na watoa huduma za mawasiliano katika hafla ya kutia saini Mkataba baina yao na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wa kupeleka huduma za mawasiliano katika vijiji 173 vilivyo katika Mikoa 16 nchini.

Amesema kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watumishi wa makampuni hayo kuchapisha taarifa binafsi za wateja na kuzitoa kwa wagomvi wao na kwa watu wasio na nia njema.

“Niwaombe sana makampuni ya simu, someni vizuri sheria, vyombo vya dola ndivyo vinavyoruhusiwa kupata taarifa binafsi za mteja kwa malengo mahsusi na sio vinginevyo”, alisisitiza Ndugulile

13 thoughts on “Watoa Huduma za Mawasiliano Wapewa onyo Kuvujisha Taarifa Binafsi za Wateja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama