Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watoa Huduma Kuhusu Ulinzi wa Minara ya Mawasiliano Wapewa Maelekezo

Na Mwandishi wetu, MTWARA

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew ametoa maelekezo kwa makampuni ya simu na wamiliki wa minara ya mawasiliano kuingia mikataba ya ulinzi wa minara ya mawasiliano na Serikali ya kijiji katika eneo husika.

Mhandisi Kundo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Newala mkoani Mtwara ya kukagua ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano ambapo alikutana na malalamiko ya malipo ya mlinzi katika mnara wa tigo uliopo katika Kijiji cha Mdimba pamoja na changamoto ya mawasiliano ya mtandao wa tigo kutokana na mnara huo kutumia nishati ya mwanga wa jua pekee

Sambamba na hilo, Mhandisi Kundo amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini ambao ndio wenyeviti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao kuhakikisha mtoa huduma yeyote mwenye mnara wa mawasiliano ndani ya wilaya zao anaandikiwa barua ya kufanya makubaliano mapya na kusainishana mikataba ya ulinzi wa minara na Serikali ya kijiji ambacho mnara upo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama