Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watendaji Acheni Urasimu kwa Wawekezaji: Rais Samia

Na Georgina Misama – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi zote nchini zinazoshughulikia masuala ya usajili wa wawekezaji kuacha tabia ya urasimu hasa kwa wawekezaji wa ndani kwani kuwachelewesha wawekezaji kunachelewesha nafasi za ajira kwa vijana, mapato ya kodi na kusababisha udumavu wa uchumi wa nchi.

Rais Samia alisema hayo leo Disemba 1, 2021 katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha kutengenezea waya kijulikanacho kwa jina la ‘Raddy Fiber’ kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, ambapo alisema kwamba urasimu kwa wawekezaji hauna nafasi katika Serkali ya Awamu ya Sita.

“Nchi yetu inahitaji wawekezaji kuliko sisi tunavyowahitaji, sisi tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyoihitaji Tanzania  hatuna budi  kufanya kila linalowezekana kuwavutia waje kwa wingi ili nchi yetu iweze kufaidika na uwekezaji wao. Tunapomchelewesha mwekezaji, tunachelewesha ajira, tunachelewesha kodi na tunadumaza uchumi wa nchi yetu,” alisema Rais Samia.

Aliongeza kwamba Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji biashara na uwekezaji ikitambua nafasi ya sekta binafsi katika mageuzi ya uchumi lengo ni kufanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi ambapo alitoa mfano wa kiwanda cha Raddy Fiber kama matokeo ya Serikali kufanya  maboresho katika mazingira ya uwekezaji.

341 thoughts on “Watendaji Acheni Urasimu kwa Wawekezaji: Rais Samia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama