Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watanzania Watakiwa Kuisaidia Serikali

Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myala akizungumza na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.

Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam

Myalla amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.
“Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi,” amesema.

Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myala akigawa daftari kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Kunguru Goba leo jijini Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.

Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais  Dk. John Pombe Magufuli katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi.

Amesema wapo wanafunzi walikuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto hiyo.

84 thoughts on “Watanzania Watakiwa Kuisaidia Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *