Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wasafiri Wanaopita Mpaka wa Tunduma Kuwekwa Karantini Siku 14

Eneo la Tunduma ambapo ni mpaka wa Tanzania na Zambia ambapo wasafiri wanao toka nchi zilizo athirika zaidi na ugonjwa wa virusi vya Corona kupitia mpaka huo watawekwa karantini kwa gharama zao kwa muda wa siku 14.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe imeanza utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kuwataka wasafiri waliotoka katika nchi zilizo athirika zaidi na maambukizi ya virusi vya Corona kukaa karantini kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao.

Jana Wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo Tunduma mkoani Songwe ili kutathmini utayari wa kuanza zoezi la kuwaweka eneo tengefu (karantini) wasafiri hao kwani mpaka wa Tunduma una watumiaji wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando akinawa mikono kwa maji yenye dawa katika mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipokagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri wanao toka nchi zilizo athirika zaidi na ugonjwa wa virusi vya Corona.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe wakinawa mikono kwa maji yenye dawa katika mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma wakati wakikagua maandalizi ya kuwaweka karantini wasafiri wanao toka nchi zilizo athirika zaidi na ugonjwa wa virusi vya Corona.

Wajumbe hao wamekubaliana kuanza mara moja zoezi hilo mbapo wasafiri hao watajitenga kwa gharama zao na kwa muda wa siku 14, ambapo zoezi hilo limeanza kutekelezwa rasmi Machi 23, 2020 usiku huku maandalizi ya maeneo na mahitaji mengine kwaajili ya kuwatenga yakifanyika.

Pia wameweka mkakati wa kufanya kaguzi mbalimbali katika nyumba za kulala wageni ili kubaini endapo kuna wageni ambao wataingia nchini kutoka nchi ambazo zimeathirika zaidi na ugonjwa wa virusi vya Corona  kwa kutumia njia zisizo halali na kisha kukwepa kukaa karantini huku ulinzi ukiimarishwa zaidi katika eneo lote la mpaka.

Aidha, wamewasihi wananchi wote kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kunawa kwa maji na sabuni, kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima kwani kinga ni bora zaidi kuliko tiba.

402 thoughts on “Wasafiri Wanaopita Mpaka wa Tunduma Kuwekwa Karantini Siku 14

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama