Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wananchi Zanzibar Waaswa Kutumia Hati za Kumiliki Ardhi Kujikwamua Kiuchumi

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA walipomtembelea Katibu huyo Ofisini kwake Forodhani mjini Zanzibar.

Na Mwandishi wetu- MAELEZO Zanzibar

Mwenyekiti wa Kamati  ya uongozi ya Ofisi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA )  Balozi mstaafu  Daniel Ole Njolay  amewataka Wananchi waliokabidhiwa Hati za Ardhi kuzitumia vyema kwa ajili ya kuombea Mikopo itakayowasaidia kupambana na umasikini wa kipato.

Balozi Njolay ametoa wito huo katika hafla ya kuwakabidhi Wananchi 54 wa Mpendae mjini Zanzibar Hati hizo mara baada ya kukamilisha masharti ya usajili.

Amesema Serikali ya Muungano  kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeazimia kuwakomboa Wananchi wake na umasikini wa kipato kupitia njia mbali mbali ikiwemo kuwapatia Hati za Ardhi zitakazowasaidia katika harakati zao za kimaendeleo.

Amewataka Wananchi hao kuzitumia Hati hizo ili kuomba Mikopo kutoka vyanzo mbalimbali vya kifedha ikiwemo Benki kwa ajili ya kuendeshea maisha yao.

“Wenzetu nje ya nchi Hati hizi zinakuwepo katika Bank huzitumia kikamilifu kukomba Mikopo ya kuwasaidia kuendeleza miradi yao ya kimaendeleo ambayo wanaianzisha hivyo  hapa Tanzania tunawajibu wa kuyaiga hayo ” amefahamisha Balozi Njolay.

Afisa Mtambuzi Ardhi Shawana Soud Khamis akizungumza na Wananchi wa Mpendae mjini Zanzibar waliokuwa wanasubiri kukabidhi wa Hat iza Ardhi zao.

Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya (MKURABITA ) Balozi mstaafu Daniel Ole Njolay akimkabidhi Bw. Said Yahya Mkaazi wa Mpendae Hati yake ya Ardhi katika hafla iliyofanyika huko Mpendae mjini Zanzibar. Kulia ni Mrajisi wa Ardhi ZanzibarDkAbdul-Nasser Hikmany

Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA Tanzania Dkt. Seraphia Mgembe amewaomba  Wananchi hao hasa Wazee kuzitumia Hati hizo ili kukamilisha ndoto zao walizoshindwa kuzifanya wakati wa ujana wao.

Amesema kabla ya kupata Hati hizo kuna mambo mengine muhimu walishindwa kuyatekeleza kwa kukosa Mikopo hivyo kupitia hati hizo wana uwezo wa kuzitumia kukamilisha ndoto zao.

Amesema ili Mwananchi awe na uchumi mzuri kunahitajika mipango endelevu itakayomsaidia kupata Mtaji wa kufikia maendeleo aliyoyajipangia.

“Inawezekana mmoja wenu alitamani kufanya mambo makubwa lakini akashindwa kwa kukosa kielelezo cha Hati ambacho kingemfanya kupata Mkopo hivyo kuanzia leo hata kama ni Mzee fursa sasa unayo ya kukopa ukafanya mambo yako unayoamini bado ni muhimu” Alishauri Dkt. Seraphia

Mzee Omar wa Mpendae kushoto akionesha Hati yake ya Ardhi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya (MKURABITA ) Balozi mstaafu Daniel Ole Njolay (katikati Mwenye Kaunda Suti) hafla ya kukabidhi hati hizo ilifanyika Mpendae mjini Zanzibar. Kuliani Mrajisi wa Ardhi Zanzibar Dk. Abdul-Nasser Hikmany.

Kwa upande wake Mrajisi wa Ardhi Zanzibar Dk. Abdul-Nasser Hikmany amewataka Wananchi waliopatiwa hati hizo kuzitumia vyema ili zilete mabadiliko ya kiuchumi kwa kuzitumia katika kutafuta Mitaji kutoka taasisi za kifedha nchini.

Amesema mwelekeo wao ni kuhakikisha maeneo yote Unguja na Pemba yanapimwa na Wamiliki wake kupatiwa Hati ambazo watazitumia kama rasilimali muhimu na kupunguza migogoro ya Ardhi.

Mmoja wa waliokabidhiwa Hati hiyo Mmanga Omar ameishukuru Serikali kwa kutoa Hati hizo ambazo zitakuwa kielelezo muhimu cha wao kupata misaada mbali mbali ya kujiendeleza na maisha.

Amesema ataitumia kama fursa muhimu ya kukopa Bank ili kuwatengenezea mustakabali mwema watoto wake ikiwemo kuwasomesha na kuwafungulia biashara.

“Pamoja na kwamba kukopa si kipaumbele sana lakini katika utaratibu uliowekwa sasa zipo Bank za Kiislam nazo zinakopesha hivyo tutazitumia ili kutengeneza future ya Watoto wetu” alisema

ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha utoaji wa Hati hizo kwa Wananchi wengine Unguja na Pemba ili kuchangamkia fursa zinazoweza kupatikana kupitia umiliki wa Hati hizo.

kupunguza  gharama za uanzishwaji wa biashara kwa wananchi ikiwemo ukataji wa Leseni ili kuyafanya mazingira ya biashara kuwa rahisi.

Awali Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA walimtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira  Ali Khalil Mirza na kumuelezea changamoto walizokutana nazo zinazodumaza maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.

Kamati hiyo ipo Zanzibar ikiendeleza ziara yake ya siku tano kukagua shughuli mbali mbali zinazofanywa na MKURABITA visiwani Zanzibar kwa lengo la kusaidia kutatulia changamoto zinazowakabili Wananchi hasa katika Nyanja za kibiashara na ardhi.

393 thoughts on “Wananchi Zanzibar Waaswa Kutumia Hati za Kumiliki Ardhi Kujikwamua Kiuchumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama