Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wananchi Wapongeza Tanzania Kutajwa Kinara Uchumi Shirikishi

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Wananchi Mkoani Dodoma wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika Kujenga uchumi  shirikishi unaogusa maisha ya wananchi baada ya Tanzania kutajwa  na Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) kuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na uchumi Jumuishi.

Akizungumza katika Mahojiano maalum mjini Dodoma Bibi Anyangwe Lupembe  amesema ni jambo la kupongeza kwa hatua hiyo kwani  haya ni matunda na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama ujenzi wa reli wa reli ya Kisasa (Standard  Gauge) na Uzalishaji umeme.

Akifafanua Lupembe amesema kuwa kila mwananchi kwa sasa anaelewa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi wanyonge kwa kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinapatikana kama Madawa, Elimu, miundo mbinu hali inayowapa fursa wananchi kushiriki katika shughuli za uchumi ikiwemo uzalishaji kutokana na mazingira wezeshi yaliyopo kwa sasa.

Aliongeza kuwa kasi ya ujenzi wa miundombinu kama  barabara inawawezesha wananchi kushiriki katika uzalishaji na shughuli za maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchi, hivyo uchumi kumilikiwa na wananchi.

Kwa upande wake Bwana George Nsavike amepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kusimamia masuala ya Kodi ambayo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ambapo kodi inayokusanywa inatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo kwa sasa inawanufaisha wananchi wote hasa wa chini.

“Rais Magufuli ameonyesha mfano mzuri katika kusimamia rasilimali za Taifa  yakiwemo madini na kusimamia ukusanyaji wa kodi ambapo wananchi wameonyesha kuunga mkono juhudi hizo ambazo zimechochea Kasi ya ukuaji wa uchumi” Alisisitiza  Nsavike

Aliongeza kuwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano upelekaji wa umeme vijijini umepewa kipaumbele hali inayowapa wananchi fursa yakushiriki katika miradi ya maendeleo.

Naye Salmin Abdalah amesema ujenzi wa miundombinu na utekelezaji wa miradi mingine umewezesha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijiletea maendeleo

Tanzania imetajwa na Jukwaa la Uchumi Duniani  (World economic Forum) kuwa nchi yakwanza Kusini mwa janga la Sahara kwa kuwa na uchumi jumuishi hivi Karibuni.

One thought on “Wananchi Wapongeza Tanzania Kutajwa Kinara Uchumi Shirikishi

  • June 23, 2021 at 1:13 am
    Permalink

    401230 416783We dont trust this remarkable submit. Nevertheless, I saw it gazed for Digg along with Ive determined you could be appropriate so i ended up being imagining within the completely wrong way. Persist with writing top quality stuff along these lines. 43658

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama