Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wananchi Kijiji cha Kalenge Waishukuru Serikali Kuwajengea Zahanati

Mkurugenzi wa idara ya tiba Dkt. Grace Magembe akiongea pembeni ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt.Zainab Chaula pamoja na wakazi wa kijiji hicho.

Na.Catherine Sungura-Uvinza

Wananchi wa Kijiji cha Kalenge wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwajengea zahanati itakayowasaidia kuwaepusha na vifo hasa vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa jana  na wakazi wa kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.

Akiongea kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata kigoma mjini.

Jengo la kujifungulia ambalo limejengwa katika zahanati hiyo

“Tunashukuru kwa serikali hii kutukumbuka Mkoa wa Kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi aende Kigoma Mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa”.

Aidha, alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa njiani.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.

“Ninawapongeza kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI na katika ziara yangu nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima utimize”, alisema Dkt. Chaula

Wakazi wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za afya karibu na wananchi.

 

2 thoughts on “Wananchi Kijiji cha Kalenge Waishukuru Serikali Kuwajengea Zahanati

 • March 23, 2021 at 4:51 am
  Permalink

  I have learn several excellent stuff here. Certainly price
  bookmarking for revisiting. I surprise how a lot attempt you place
  to make such a wonderful informative site.

  Reply
 • July 5, 2021 at 3:03 pm
  Permalink

  766853 330500Its actually a cool and beneficial piece of info. Im glad that you shared this valuable data with us. Please keep us informed like this. Thanks for sharing. 760893

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama