Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wakulima Uyui Kuongeza Uzalishaji wa Alizeti na Pamba Msimu Ujao

Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Uyui kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kujengewa uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Lutende na kukabidhiwa hati miliki za kimila jana.

Na Tiganya Vincent

WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) wameazimia kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti na pamba kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuvutia wawekezaji katika sekta ya viwanda.

Azimio hilo limefikiwa jana na Wakulima 200 na viongozi 20 wa vijiji vya Miyenze na Lutende wilayani Uyui baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA).

Akisoma maazimio ya wakulima Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema wakulima wamekubaliana kulima ekari sita(6) za alizeti na ekari tatu za pamba na mazao ya chakula kwa ajili ya kuinua uchumia wao.

Alisema ongezeko hilo la kilimo linakwenda sanjari na mtumizi ya mbegu za kisasa za alizeti na kulima kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuwa na malighafi nyingi zitakazovutia wawekezaji kwenda Uyui.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lutende wilayani Uyui wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na kukabidhiwa hati miliki za kimila jana yaliyokuwayameandaliwa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).

Aidha wakulima hao pia walikubaliana kuanza kuwa na kilimo biashara kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo chao na kuondokana na umaskini unatokana na uzalishaji wa mazoea wa uzalishaji wa kujikimu na kuelekea katika uzalishaji wa ziada.

Katika hatua nyingine wamekubaliana kuanzisha chama cha Ushirika wa Wafugaji ili wawezeze kuunganisha nguvu pamoja katika kutafuta huduma mbalimbali ikiwemo ya kupata dawa za mifugo kwa urahisi na uuzaji wa bidhaa za mifugo kwa bei nzuri.

210 thoughts on “Wakulima Uyui Kuongeza Uzalishaji wa Alizeti na Pamba Msimu Ujao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama