Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu 3,200 Wanufaika na Mafunzo ya Vitendo Sehemu za Kazi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waajiri na Vijana wanufaika wa Mafunzo ya Vitendo sehemu za Kazi “Internship Training” alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mafunzo wanayopatiwa vijana hao na waajiri, Mkoani Iringa.

Na. Mwandishi Wetu – Iringa

Vijana wahitimu wa Vyuo vya elimu ya juu zaidi ya 3,200 nchini wamenufaika na Mafunzo ya vitendo mahala pa kazi “Internship Training” yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira ambapo zamani ilikuwa ni Wakala wa Huduma za Ajira (TAESA).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa katika ziara Mkoani Iringa kutembelea waajiri wenye vijana wanaowapatia mafunzo katika sehemu zao za kazi yaani “Interns”.

Waziri Mhagama alieleza kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakihusisha vijana waliohitimu ngazi mbalimbali za elimu ambapo wanapatiwa fursa ya kujifunza kwa vitendo katika maeneo ya kazi kwa lengo la kuwapatia uzoefu wa kazi utakaowasaidia kuajiriwa au kujiajiri.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa taarifa kuhusu Mafunzo ya Vitendo sehemu za Kazi “Internship Training” kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mafunzo wanayopatiwa vijana hao na waajiri katika mkoa huo.

“Kuanzishwa kwa mafunzo hayo ilikuwa ni moja kati ya maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana hususani kwenye masuala ya ajira nchini, hivyo vijana waliomaliza kozi mbalimbali kupatiwa ujuzi katika maeneo ya kazi ili waweze kuwa na uzoefu pale wanapojiajiri ama kuajiriwa,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa Mpango huu wa mafunzo ya vitendo mahala pa kazi umekuwa na mchango mkubwa na ni chachu katika kuwezesha nguvukazi ya taifa hususan vijana waliohitimu kwa kuwajengea uzoefu, weledi na maadili ya kazi yanayohitajika pindi wanapoajiriwa.

“Tunataka kuona vijana wanapomaliza mafunzo haya wanakuwa na dhana ya kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu hii ya tano kwa kuwa tayari mnauzoefu,” alisema Mhagama.

Sehemu ya Vijana wanufaika wa Mafunzo ya Vitendo sehemu za Kazi “Internship Training” wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).

“Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya tathmini ya mafunzo haya na mafunzo mengine yanayotolewa chini ya Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ili kuona namna ujuzi wanaopatiwa vijana nchini unakuwa wa manufaa katika kuwezesha vijana wanakuwa sehemu ya kufikisha taifa lao katika uchumi wa kati,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama alitoa wito kwa vijana ambao wamenufaika na mafunzo hayo kufanya kazi kwa bidi, weledi na maarifa kwa kuonyesha umahiri wa kujenga uchumi wa taifa.

Sambamba na hayo, alitoa pongezi kwa waajiri wote nchi katika sekta ya Umma na Binafsi kwa namna walivyoshirikiana na Serikali katika kuwapatia vijana mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita hadi mwaka mmoja na wamekuwa sehemu ya mafanikio katika kuziwezesha taasisi kufikia malengo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alieleza kuwa Programu hiyo ya mafunzo kwa Vitendo sehemu za Kazi imekuwa na manufaa makubwa kwa vijana na ameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha ujao kutenga bajeti zaidi kwa ajili ya kuwezesha vijana wanaohitimu kwenye vyuo mbalimbali nchini ili waweze kunufaika na mafunzo hayo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa GIBRL Business Solutions Ltd, Bi. Hadija Jabir alisema kuwa uwepo wa vijana wanaopatiwa mafunzo hayo katika kampuni yake umekuwa na tija.

“Kama mwajiri nimeona ufanisi wa vijana hao, naiomba serikali iwapatie nafasi zaidi ya vijana hao wanaohitimu kufanya mafunzo katika sehemu za kazi ili yale waliyojifunza kwa nadharia waweze kuyatekeleza kwa Vitendo,” alisema Jabir

Naye, Mmoja wa Wanufaika wa Mafunzo hayo, Bi. Felister Gerald ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wa vijana na kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewasaidia kuwajengea uzoefu na ujasiri wa kufanya kazi.

8 thoughts on “Wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu 3,200 Wanufaika na Mafunzo ya Vitendo Sehemu za Kazi

 • August 11, 2020 at 1:01 am
  Permalink

  Remarkable things here. I am very satisfied to peer your post.

  Thanks a lot and I am having a look ahead to contact you.
  Will you please drop me a mail?

  Reply
 • August 11, 2020 at 12:01 pm
  Permalink

  We’re a group of volunteers and starting a new scheme in our community.
  Your web site provided us with useful info to work on. You’ve performed a formidable
  job and our whole neighborhood shall be grateful to you.

  Reply
 • August 11, 2020 at 5:20 pm
  Permalink

  When some one searches for his necessary thing, therefore he/she desires to be available that in detail, thus that thing
  is maintained over here. adreamoftrains best web hosting company

  Reply
 • August 14, 2020 at 12:17 am
  Permalink

  Your method of describing everything in this paragraph is
  actually pleasant, every one can easily know it, Thanks a lot.

  Reply
 • August 24, 2020 at 3:15 pm
  Permalink

  Hi there just wanted to give you a quick heads
  up. The words in your post seem to be running off the
  screen in Internet explorer. I’m not sure if this is a format issue or something to do with
  internet browser compatibility but I thought I’d post to let you
  know. The design look great though! Hope you get the issue fixed soon.
  Thanks 3aN8IMa cheap flights

  Reply
 • August 25, 2020 at 9:27 pm
  Permalink

  Thanks to my father who told me concerning this
  blog, this webpage is genuinely awesome. cheap flights 2CSYEon

  Reply
 • August 28, 2020 at 5:07 am
  Permalink

  Hello! Would you mind if I share your blog
  with my zynga group? There’s a lot of people that I think would really appreciate your content.
  Please let me know. Many thanks

  Reply
 • August 31, 2020 at 7:52 am
  Permalink

  This website was… how do I say it? Relevant!! Finally I have found something
  which helped me. Kudos!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *