Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wadau wa Maendeleo Kuchagia Bilioni 98.1 Kupitia Mfuko wa Afya wa Pamoja

Na Englibert Kayombo, WAF – Dar es Salaam

Wadau wa Mfuko wa Afya wa pamoja nchini (Health Basket Fund) wamepanga kuchangia kiasi cha shilingi Bilioni 98.1 kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2022/2023.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha kujadili uboreshaji wa mfuko huo kupitia ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali na wadau Jijini Dar Es Salaam.

“Kwa niaba ya Serikali, tunawashukuru wadau wetu wanaochangia kwa pamoja kwenye Mfuko wa Afya na tunatarajia kwa Mwaka wa fedha ujao wa 2022/23 wadau wetu kwa pamoja kuchangia Shilingi bilioni 98.1 na fedha hizo zitaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti za Vituo vya kutolea huduma za Afya nchini”, amesema Waziri Ummy Mwalimu.

65 thoughts on “Wadau wa Maendeleo Kuchagia Bilioni 98.1 Kupitia Mfuko wa Afya wa Pamoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama