Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wabunge Waikubali Bajeti ya Serikali

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Na: Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamezidi kuiunga mkono bajeti ya serikali iliyowasilishwa bungeni mapema wiki liyopita.

Akitoa maoni yake katika mahojiano maalum na Idara ya Habari – MAELEZO, Mbunge wa Kaliua (CUF), Mhe. Magdalena Sakaya amesema bajeti hii ni nzuri kwani imeondoa tozo na ushuru ambavyo vilikuwa vikiwakera wananchi zikiwemo za taulo za akina mama na mabinti.

Mbunge huyo ameungamkono bajeti hiyo kwa kuishukuru Serikali kwa kujenga miradi mikubwa ya kuboresha miundombinu ukiwemo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge).

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akijibu swali wakati kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangala wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

“Kwa kweli naipongeza Serikali kwa kujenga miundombinu ya reli na barabara kwani ujenzi wa uchumi wa viwanda bila miundombinu bora haiwezekani, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler’s Gorge unaonyesha dhahiri jinsi Serikali ilivyo makini kwenye utendaji wake”, alisema Sakaya.

Naye Mbunge wa Pangani, Mhe. Jumaa Aweso katika mahojiano hayo amesema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu ya reli, maji na barabara kwani itasaidia juhudi za Serikali za ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda.

Aweso amesema Serikali inapojenga barabara na kuimarisha miundombinu ya maji itasaidia kuboresha kilimo hasa cha umwagiliaji kwani kilimo kitaweza kuwa chenye tija badala kilimo cha kizamani cha kutegemea hali ya hewa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akijibu swali wakati kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa Msafiri (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Anne Kilango Malecela wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

“Niseme wazi bajeti hii ni nzuri sana kwani inagusa maisha ya wananchi kwani imewaondolea kero za muda mrefu na itawafanya waweze kuongeza vipato kutokana na kuwekwa mazingira mazuri ya uwekezaji”, alisema Aweso.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mvomero, Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq amesema bajeti hii ni nzuri kwani imebuni vyanzo vipya vya mapato badala ya vilivyozoeleka vya kuongeza ushuru kwenye sigara, bia na soda.

Mhe. Sadiq amesema serikali imefanya vizuri kwa kupunguza kodi kwenye viwanda vya kutengeneza bidha a za ngozi ili kuchochea uwekezaji katika viwanda vya aina hiyo nchini.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akijibu swali wakati kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki, Mhe. Gudlucky Millinga akiomba muongozo wa Spika wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Madini, Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Mbunge wa Geita Vijijini, Mhe. Joseph Kasheku Msukuma wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) wakati majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa taifa, mpango wa maendeleo wa mwaka 2018/19 na mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 katika kikao cha 11 cha mkutano wa Bunge la 52 leo tarehe 19 Juni 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

Baadhi ya wageni wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ambao ni Wabunge kutoka nchini Afrika Kusini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo tarehe 19 Juni 2018 Jijini Dodoma. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)

Mbunge huyo amependekeza kuwa ushuru upunguzwe pia kwenye zana za kilimo ili kilimo kiweze kuwa cha kisasa na chenye tija.

Akitoa maoni yake kuhusu bajeti ya Serikali, Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Edward Franz Mwalongo kuwa bajeti imekaa vizuri kwani inajenga uchumi imera kutokana na kujenga miundombinu imara ikiwemo ya Standard Gauge na ule wa umeme wa Stiegler’s Gorge.

Mwalongo amesema kuwa miundombinu bora itasaidia kutoa mazao shambani hadi sokoni na hivyo kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Wabunge wanaendelea kuchangia bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kama livyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.

5 thoughts on “Wabunge Waikubali Bajeti ya Serikali

 • August 12, 2020 at 6:14 am
  Permalink

  Very good information. Lucky me I ran across your blog by accident (stumbleupon).
  I’ve bookmarked it for later! adreamoftrains web hosting company

  Reply
 • August 24, 2020 at 11:58 pm
  Permalink

  Good day! I know this is kind of off topic but I was wondering if you knew where I could locate a captcha plugin for my
  comment form? I’m using the same blog platform as yours and I’m having trouble finding one?

  Thanks a lot! cheap flights 32hvAj4

  Reply
 • August 25, 2020 at 7:11 pm
  Permalink

  This web site really has all of the information I wanted concerning this subject and didn’t know who to
  ask. 3gqLYTc cheap flights

  Reply
 • August 31, 2020 at 9:33 pm
  Permalink

  Its like you read my mind! You appear to know a lot about this, like you wrote the book in it or something.
  I think that you could do with some pics to drive the message home a bit, but other than that, this is wonderful blog.
  A fantastic read. I will certainly be back.

  Reply
 • September 5, 2020 at 9:18 am
  Permalink

  What’s up to every one, as I am in fact keen of reading this web site’s post to be updated on a regular basis.
  It includes fastidious material.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *