Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wabunge Vinara Waahidi Kushirikiana na Serikali Kukemea Vitendo vya Ukatili


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akifungua kikao hicho, amewapongeza wabunge kwa hatua ya makusudi kuamua kuunda kikundi cha vinara kwa ajili ya kusaidia Jamii katika suala la ukatili wa kijinsia kuhakikisha unakwisha.


Mhe. Mwanaidi amewaomba Wabunge hao kutoa elimu kuhusu ukatili wowote na madhara yake na kuwaeilimisha wananchi kushiriki katika kutoa ushahidi mahakamani kwa wanaokabiliwa na vitendo hivyo.


Ameongeza kwamba bado kuna upungufu wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri hali inayochangia utoaji wa Huduma za Ustawi kutopatikana kwa urahisi.


“Huduma za Ustawi wa Jamii zinahitaji kufikia  Jamii na Makundi yenye mahitaji maalum kwa wakati ili kutatua changamoto zinazowakabili ili washiriki kikamilifu katika Ustawi na Maendeleo ya Taifa, hata hivyo kuna idadi ndogo ya Maafisa Ustawi wa Jamii wanaopaswa kusaidia na kutoa huduma hizo” amesema Mhe. Mwanaidi.


Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Afya, lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe amewashukuru Wabunge vinara kwa kuisaidia Serikali kusukuma mbele masuala ya Ustawi wa jamii tangu kikundi cha Wabunge hao vinara kianzishwe mwaka 2021

.
Dkt.  Kapologwe amesisitiza uhitaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii ni mkubwa na kwamba Serikali inazingatia na kulipa uzito suala hilo.
“Katika kibali cha ajira ambacho tutaajiri watumishi wa Afya 7612 ndani yake kuna Maafisa Ustawi wa Jamii na Maaafisa lishe ambayo itasaidia sana kupynguza changamoto iliyopo” amesema Dkt. Ntuli.


Aidha, amesema kupitia ajira zilizopitishwa na Mhe. Rais Samia matarajio ni kuwa Maafisa Ustawi wa Jamii katika vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya kwenye kila Halmashauri ambayo itasaidia kupambana na vitendo vya ukatili na Masuala ya ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mimba za utotoni.

Awali akieleza lengo la kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii, Joseph Kahinga amebainisha kwamba wabunge wakipata uelewa wataweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utekelezaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii kwa kupaza sauti katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama