Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waandishi wa Habari Nchini Waaswa Kuzingatia Maadili

 

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Balozi Hebert Mrango akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo kwa mwandishi wa habari yanayolenga kujenga uwezo kwa waandishi hao ili waweze kuandika na kuripoti habari za SADC kwa maslahi ya wananchi wa nchi wanachama.

Na; Frank Mvungi- Morogoro

Waandishi wa Habari nchini wameaswa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo wakati wa kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa lengo la kuchochea ustawi wa wananchi wa nchi wanachama hasa fursa zilizopo.

Akizumzunza wakati akifunga mafunzo ya kundi la kwanza la waandishi wa habari watakaoripoti na kuandika habari za SADC leo mjini Morogoro Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Balozi Hebert   Mrango amesema kuwa, kila mwandishi analojukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu jumuiya hiyo na kwa wakati ili waweze kutumia fursa ya soko lililopo katika nchi 16 wanachama.

“Nchi za SADC zina soko kubwa linaloweza kuchangia katika kukuza uchuni wa nchi wanachama hivyo hii fursa ya kujitangaza wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wananchama na Serikali” Alisisitiza Balozi  Mrango.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt Ayub Rioba akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yanayofanyika mjini Morogoro ili kuwawezesha kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwa ni siku ya tatu na ya mwisho kwa kundi la kwanza la washiriki wa mafunzo hayo leo Julai 10, 2019.

Akifafanua amesema kuwa nchi wanachama  ikiwemo Tanzania zina fursa ya kutangaza bidhaa zinazozalisha hasa zinazotokana na sekta ya Kilimo na Viwanda ili kuchochea ukuaji wa sekta hizo .

Kwa upande wake mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustiono  Tanzania (SAUT) Dkt. Kaanaeli  Kaale amesema kuwa kila mwandishi wa habari analo jukumu la kuhakikisha kuwa mwenendo wake unaendana na taratibu zote zinazosimamia taaluma hiyo kwa maslahi ya  nchi wanachama wa SADC.

“ Habari zinazoandikwa na kuripotiwa zinapaswa kulenga kujenga SADC na Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia  usahihi, ukweli, kufanya uchunguzi na kujiandaa vyema wakati wa kufanya mahojiano na Viongozi mbalimbali watakaoshiriki mkutano wa 39 wa Wakuu wa  nchi na Serikali za nchi wanachama” Alisisitiza Dkt Kaale

Akifafanua amesema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa  na uelewa kuhusu manufaa ya Jumuiya hiyo na mchango wake katika kuleta ustawi wa wananchi.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo kwa waandishi wa habari yanayolenga kuwawezesha kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayofanyika mjini Morogoro ikiwa ni siku ya tatu, hayo yamejiri Julai 10, 2019.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba amesema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kujenga uelewa kuhusu masuala yanayogusa nchi wanachama wa SADC kwa maslahi ya wananchi.

Aliongeza kuwa falsafa ya SADC imejikita katika mambo yanayolenga kuleta ustawi kwa wananchi unaojikita  kwenye; Utu, uhuru, usawa, haki na umoja ili kuchochea maendeleo ya nchi wanachama wa SADC.

“Mafunzo haya yanalenga kujenga uwezo zaidi kwa waandishi wa habari ili watumie weledi kuandika na kuripoti habari za SADC na fursa zilizopo zitakazowanufaisha wananchi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yanayofanyika mjini Morogoro leo Julai 10, 2019 ikiwa ni siku ya tatu, Lengo likiwa kuwawezesha kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) .

Akifafanua amesema kuwa waandishi hao wanapaswa  kuzingatia utamaduni wa  nchi wanachama  wa SADC wakati wote kwa maslahi ya Jumuiya hiyo .

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Kimatifa la Maendeleo la Ujerumani lililofadhili mafunzo hayo kupitia SADC, Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Dagmore Tawonezvi amesema kuwa wanamatumaini kuwa habari zinazohusu SADC zitaandikwa na kuripotiwa kwa maslahi ya wananchi wote.

Aidha, Bw. Tawonezvi aliongeza kuwa Shirika hilo limejipanga kuwa na tuzo kwa waandishi wa habari na katika ngazi ya shule ili kuhamasisha utoaji na utangazaji wa habari za maendeleo za SADC.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari  yanayolenga  kuwawezesha kuwa na weledi wa kutosha katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Mshiriki wa Mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka Shirika la Utangzaji la Uingereza (BBC) Bw. Abubakar Famau akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo yanayolenga kuwawezesha kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ili kuwajengea wananchi uelewa kuhusu fursa zinazotokana na Jumuiya hiyo, hayo yamejiri Julai 10, 2019 mjini Morogoro.

Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akisisitiza umuhimu wa kutumia fursa zinazotokana na mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC ili kuchochea maendeleo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) Dkt. Kaanaeli Kaale akisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia maadili wakati akiwasilisha mada katika mafunzo yakuwajengea uwezo yanayofanyika mjini Morogoro ili kuongeza weledi utakaowawezesha kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwa ni siku ya tatu na mwisho kwa kundi la kwanza la washiriki wa mafunzo hayo leo Julai 10, 2019.

(Picha na Abubakari  W.  Kafumba)

7 thoughts on “Waandishi wa Habari Nchini Waaswa Kuzingatia Maadili

 • August 11, 2020 at 12:22 am
  Permalink

  It’s actually very complex in this full of activity
  life to listen news on TV, so I just use internet for that purpose, and obtain the newest information. adreamoftrains web hosting companies

  Reply
 • August 11, 2020 at 8:47 am
  Permalink

  Your style is unique compared to other people I’ve read stuff from.
  Thanks for posting when you’ve got the opportunity, Guess I’ll just bookmark this
  blog.

  Reply
 • August 25, 2020 at 5:01 am
  Permalink

  Hello friends, how is everything, and what you want to say concerning this article,
  in my view its really awesome in support of me.
  cheap flights 3aN8IMa

  Reply
 • September 5, 2020 at 12:43 pm
  Permalink

  Hi would you mind letting me know which web host you’re utilizing?
  I’ve loaded your blog in 3 different internet browsers and I must say this blog loads a lot quicker then most.
  Can you recommend a good hosting provider at a fair price?
  Cheers, I appreciate it!

  Reply
 • June 21, 2021 at 8:21 am
  Permalink

  Hello, I think your web site might be having web browser compatibility problems.
  When I take a look at your web site in Safari, it looks fine however, if opening in Internet
  Explorer, it has some overlapping issues. I merely wanted to provide you with a quick heads up!
  Apart from that, wonderful website!

  Reply
 • June 30, 2021 at 10:00 pm
  Permalink

  I’ve read some good stuff here. Definitely price bookmarking for revisiting.
  I surprise how a lot effort you place to make the sort of magnificent informative web site.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama