Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vyuo Vilivyo Chini ya Wizara ya Fedha Vyaagizwa Kuongeza Tafiti

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni, amekiagiza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) kufanya tafiti zitakazo ibua vyanzo vipya vya mapato na kodi ili kuisaidia Serikali katika kutekeleza mipango ya maendeleo kwa watanzania.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam alipotembelea Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya vyuo hivyo katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama