Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

VIKWAZO 174 VYA BIASHARA EAC VIMEONDOLEWA KWA WAFANYABIASHARA

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.Sekela Mwaisela akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.Sekela Mwaisela, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi Wetu-MAELEZO

Jumla ya vikwazo 174 sawa na asilimia 75 vimeondolewa ili kurahisisha ufanyaji biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo sasa itawezesha kuwepo kwa biashara kubwa baina ya nchi hizo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Mkutano kati ya Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara, Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya Mtangamano wa Biashara, Bi.Sekela Mwaisela alisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kanda zingine kuna sheria ambazo zinazingitia biashara.

“Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ibara ya 13(1) Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Biashara pamoja na Ibara ya 6 ya Itifaki ya Biashara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika (SADC) zinazitaka Nchi Wanachama kuondoa vikwazo vya zamani ili kuwezesha biashara kwa wafanyabiashara”, Alisema Mwaisela.

Afisa Biashara Kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Mpanduji Mathias akifafanua jambo kwa Wafanyabiashara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwaisela alieleza kuwepo kwa juhudi za kuondoa kabisa vikwazo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikishirikisha kuwepo kwa vikao vya kamati za biashara, Mikutano ya Kikanda, Mikutano ya Mawaziri pamona na Mikutano ya Nchi kwa Nchi hiyo itatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoa changamoto zao kwa utatuzi zaidi.

Katika kuteleza hilo Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wadau leo imefungua Mkutano wa wadau wa biashara ambapo agenda kubwa ni kuelimisha wafanyabiashara kuhusu kutoa taarifa iwapo watakutana na vikwazo mbalimbali wakiwa kwenye kusafirisha bidhaa zao.

“Kusudi kubwa la Mkutano huu leo ni kujadiliana kuhusu kutoa vikwazo lakini pia kuwawezesha wafanyabiashara kuwa na elimu kuhusu hivyo vikwazo wanavyokutana navyo, sehemu gani ya kutoa taarifa kwa Msaada Zaidi”, alisema Mwaisela.

Afisa Biashara Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Aneth Simwela akifafanua jambo kwa Wafanyabiashara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu akifafanua jambo kwa Wafanyabiashara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wafanyabiashara na Kamati ya Taifa inayoshughulikia vikwazo vya biashara kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Alisema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kujenga miundombinu wezeshi ikiwemo Bandari, Reli, ambavyo vinaambana na ujenzi wa miradi mikubwa kama ule wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme Julias Nyerere Hydro Power Poject (JN HPP) ambao utazalisha Megawati 2,115.

Kwa upande wa wadau wa biashara wao wamesema kuwa Serikali imewezesha kuwepo kwa mazingira mazuri ya biashara katika Jumuiya ya Nchi wanachama ukiachilia mbali kuwepo kwa vikwazo vidogovidogo ambavyo vinatatulika.

“Mkutano huu unaonesha nia njema ya Serikali kuweza kuwasiliana kwa karibu na wafanyabiashara ili kuweza kujua changamoto zao na mazingira ya biashara wanayokutana nayo sokoni, tumefurahi kwamba Serikali imejitahidi kupunguza changamoto za biashara” David Minja, Unilever.

234 thoughts on “VIKWAZO 174 VYA BIASHARA EAC VIMEONDOLEWA KWA WAFANYABIASHARA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama