Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vijana Nchini Wametakiwa Kutumia Muda Vzuri Ili Kufikia Malengo Waliyojiwekea

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri Wambura ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la Miss Garden Route 2017/2018  Mei 6 mwaka huu nchini humo katika mji wa George.

Mlimbwnde Witness aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.

“Ni dhahiri umetumia ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na sheria ambavyo umevipata  kutoka kwa familia, jamii ya Kitanzania na pia kwa jamii ya watu wa  Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.

“Vijana wa Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.

Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.

Hatua hiyo inaonesha Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali kutumia muda wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake la msingi nchini humo ni la Kimasomo.

Zaidi ya hayo Naibu Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo inatambulisha utamaduni, kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa kuongeza juhudi, maarifa na kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta matokeo mazuri yenye tija.

Aidha, Naibu Waziri Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza kipato na kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake yeye binafsi na kwa Taifa.

Kwa upande wake Miss Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa anajivunia kuwa Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri Watanzania kusimama kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mashindano ya Miss Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel Bay Afrika Kusini.

20 thoughts on “Vijana Nchini Wametakiwa Kutumia Muda Vzuri Ili Kufikia Malengo Waliyojiwekea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *