Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vijana Kuwezeshwa Ufugaji Kibiashara

Na Mbaraka Kambona, Dodoma

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameitaka taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) na taasisi inayoshughulika na kilimo biashara (PASS) kupitia mradi wanaoutekeleza wa  kunenepesha mbuzi kuhakikisha vijana wengi wanapata ujuzi huo ili waweze kuwa na fursa pana ya ajira na kukuza uchumi wao .

Ulega alitoa maelekezo hayo katika kikao kazi cha kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kunenepesha mbuzi unaotekelezwa kwa ushirikiano na taasisi hizo mbili kilichofanyika jijini Dodoma Jana.

Alisema mradi huo ni lazima ujikite katika kuwasaidia vijana wengi kupata ujuzi wa kufuga kibiashara na kuwawekea mfumo mzuri utakaowasaidia kuwezeshwa kifedha ili wawe na mitaji ya kutosha kuendesha biashara ya mifugo.

“Tunataka tutoe ajira kwa vijana, hivyo ni lazima kuwatengeneza vijana wengi watakaokuwa na ujuzi wa kunenepesha mifugo, sasa hivi wanaofanya unenepeshaji wapo na wanawezeshwa na benki zetu, lakini tunataka tupate vijana wengi zaidi watakaotengenezwa kupitia mradi huu, tukiweka nguvu yetu hapo vizuri naamini tutawezesha vijana wengi kujiajiri,”alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama