Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vijana 240 Kuwezeshwa Kujiajiri Sekta ya Mifugo

Na Mbaraka Kambona

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuanzia mwaka huu wa fedha 2022/23 Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) na Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) imeanzisha vituo atamizi nane (8) ambavyo vitahusisha vijana 240 waliohitimu taaluma za mifugo kwa ajili ya unenepeshaji mifugo katika vituo vilivyopo katika Mikoa ya Tanga, Kagera, Songwe na Mwanza.

Waziri Ndaki alisema hayo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki katika taarifa yake kwa umma kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za Wakulima (NaneNane) yaliyofanyika jijini Mbeya Agosti 8, 2022.

“Nimeziagiza taasisi hizo kuanza ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo mara moja na kukamilisha taratibu za kuwapatia vijana”, alisema Ndaki.

2 thoughts on “Vijana 240 Kuwezeshwa Kujiajiri Sekta ya Mifugo

  • August 15, 2022 at 11:03 am
    Permalink

    First of all, thank you for your post. majorsite Your posts are neatly organized with the information I want, so there are plenty of resources to reference. I bookmark this site and will find your posts frequently in the future. Thanks again ^^

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama