Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Mnara wa Tanki la Maji Kilimani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mnara wa Tanki la Maji Safi na Salama katika eneo la Kilimani Mnara wa Mbao Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Ndg.Mussa Ramadhan Haji, akitowa maelezo ya ujenzi wa Mradi Mnara wa Tanki la Maji katika eneo la Mnara wa Mbao Kilimani akiwa katika ziara yake Wilaya ya Mjini Unguja,kushoto kwa Rais Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Waziri wa Ardhi.Maji Nishati na Makaazi Zanzibar. Mhe. Salama Aboud Talib

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Mradi ya Ujenzi wa Tanki Jipya la Maji linalojengwa Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar


FacebooktwittermailFacebooktwittermail