Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ushirikiano Ndio Njia Muhimu Katika Kupata Takwimu Sahihi – Makamba

Na Adelina Johnbosco: MAELEZO, Dodoma

Tanzania ili iweze kufikia hatima ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi , ofisi ya Taifa ya takwimu ishirikiane vyema na taasisi pamoja na mashirika ya utafiti katika kuhakikisha tafiti zinazofanyika zinatoa takwimu sahihi.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati wa uzinduzi wa semina ya wadau kuhusu uanzishwaji wa ushirikiano wa Kitaifa na Kimataifa wa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa takwimu za mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi.

”Ripoti zifanane, vitu vyote vyaweza kuharibiwa lakini sio takwimu, kwani ndio kioo cha kila jambo duniani, utofauti ukionekana kwenye ripoti itakwamisha wadau na serikali kwenye mipango ya maendeleo,” amesema Makamba

Mbali na ushirikiano, amesisitiza watafiti kujengeana uwezo katika kuhifadhi na kuchambua takwimu ili kufikisha ujumbe kwa walengwa, kwani uchambuzi huo huchangia maamuzi sahihi ya mipango ya maendeleo.

Aidha, ameitaka ofisi ya Taifa ya Takwimu na wadau wengine wa kitaifa na kimataifa katika masuala ya tafiti kuhusu mazingira, wajikite katika kutoa elimu kwa umma juu ya visababishi na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, kwani uhafifu wa uelewa juu ya mazingira unasababisha wananchi kuwa vyanzo vikuu vya tatizo.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, amesema lengo kuu la takwimu za tafiti juu ya mazingira ni kuhakikisha zinapatikana taarifa rasmi ili kuwasaidia watunga sera nchini na duniani kote katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Kama takwimu zikiwa sahihi, na za kutosha, tatizo la tabia ya nchi litakomeshwa kwani hakutakuwepo na mkanganyiko wa kujiuliza ni nini sababu kuu ya tatizo wakati kila kitu kitakuwa wazi,” amesema Dkt. Chuwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Taifa cha Takwimu Benedict Mugambi, akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, amesema, kuna uhusiano mkubwa kati ya watu, mazingira na uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi, hivyo watu wanapaswa kuelimishwa juu ya utunzaji wa mazingira mahali wanapoishi.

”Katika sensa ya watu na makazi sehemu yenye watu wengi kuna uharibifu zaidi wa mazingira unaopelekea uwepo wa mabadiliko ya tabia ya nchi kuliko penye watu wachache,” amesema Mugambi

Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Serikali ya Ujerumani (GIZ), Samwel Sudi amesema takwimu za mazingira zikitumika vyema zinachagiza uwepo wa maendeleo, kwani taarifa hizo zinasaidia wadau wa maendeleo na serikali kutekeleza mambo mbalimbali yanayohusu mabadiliko ya tabia ya nchi.

”Tunajitahidi kuweka mikakati ya kuhakikisha ulimwenguni kote tunakuwa na njia za kuzuia uharibifu wa mazingira unaosababisha mabadiliko mbalimbali ya nchi ikiwemo mafuriko, ukame na hewa chafu, hii itasaidia kuwepo kwa maendeleo katika nyanja zote” amesema Victor Ohuruogu Mwakilishi kutoka Ushirikiano wa Kimataifa wa Takwimu kwa Maendelelo Endelevu (Global Partinership for Sustainable Development Data- GPSDD)

Suala la mazingira na hali nzuri ya tabia ya nchi si la nchi moja pekee, wakati Tanzania ikiweka mikakati ya kutumia takwimu kukabiliana nalo, wadau wa kimataifa nao wanalipigania kuhakikisha duniani kote hali inatengamaa.

 

8 thoughts on “Ushirikiano Ndio Njia Muhimu Katika Kupata Takwimu Sahihi – Makamba

 • August 11, 2020 at 7:01 pm
  Permalink

  Oh my goodness! Awesome article dude! Thank you, However I am going through troubles with your RSS.
  I don’t know why I am unable to join it. Is there anybody getting the same RSS problems?
  Anyone that knows the answer will you kindly respond?
  Thanks!!

  Reply
 • August 12, 2020 at 7:08 am
  Permalink

  It’s an awesome paragraph in favor of all the internet people; they will get advantage from it
  I am sure. adreamoftrains best hosting

  Reply
 • August 14, 2020 at 12:51 am
  Permalink

  Hey there! Someone in my Myspace group shared this site with us so I came to give it
  a look. I’m definitely enjoying the information. I’m book-marking and will be tweeting this to
  my followers! Excellent blog and superb design.

  Reply
 • August 25, 2020 at 12:29 am
  Permalink

  Its like you learn my thoughts! You seem to grasp a lot approximately this, such as you wrote the e book in it or something.
  I think that you simply could do with a few % to force
  the message house a little bit, but instead of that, that is magnificent blog.
  An excellent read. I will certainly be back. 31muvXS cheap flights

  Reply
 • August 25, 2020 at 3:59 pm
  Permalink

  Thanks for ones marvelous posting! I definitely enjoyed reading it,
  you could be a great author. I will remember to bookmark your blog and definitely will come back down the road.
  I want to encourage yourself to continue your great work, have a nice morning!

  Reply
 • August 27, 2020 at 9:30 am
  Permalink

  Hello there, just became aware of your blog through Google, and found that
  it’s really informative. I’m gonna watch out for brussels.
  I will appreciate if you continue this in future.
  Many people will be benefited from your writing.
  Cheers!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *