Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

UPU Wakubaliana Malipo ya Gharama Mpya za Kusafirisha Vifurushi na Mizigo

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 3 wa Dharura wa UPU Dk. Jim Yonazi akisainiMakubalioano ya Malipo mapya ya kusafirisha Vifurushi huko Geneva, Switzerland.Wakishuhudia kutoka kushoto; Ms Neema Manongi (Afisa Itifaki wa UN Ofisi ya Geneva), Bw.. Elia Madulesi, Mkuu wa Uhusiano Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Haruni H. B. Lemanya, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Na Innocent Mungy – WUUM-M

Mkutano wa 3 wa Dharura wa Baraza Kuu la Umoja wa Posta Duniani (UNIVERSAL POSTAL UNION) umefanyika jijini Geneva, Switzerland, kuanzia tarehe 24 hadi 26 mwezi Septemba, 2019, umekubaliana gharama mpya za malipo za usafirishaji wa barua, vifurushi, vipeto na mizigo kjwa nchi wananchama wa umoja huo.

Tanzania ilihudhuria mkutano huo, ikiwa na ujumbe uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu-Mawasiliano, Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jimmy Yonazi pamoja na wajumbe wengine kutoka Shirika la Posta nchini (TPC) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA.

Nchi wananchama wa Umoja UPU waliohudhuria Mkutano huo walifikia makubaliano kuhusu malipo ya gharama mpya za kusafirisha vifurushi za kimataifa, zikiwa zimezingatia gharama za uendeshaji wa kupokea, kuhifadhi na kusafirisha hadi kufikisha vifurushi hivyo bila kuleta hasara kwa Posta itakayofanya kazi hiyo. Gharama hizo ni zilipendekezwa na nchi wanachama wa UPU wakati wa Mkutano Mkuu wa wa UPU wa mwaka 2016 (Universal Postal Congress) uliofanyika Instanbul Uturuki.

Mnamo tarehe 17 Oktoba, 2018, Marekani ilipeleka barua UPU kujitoa kwenye umoja wa Posta Duniani (UPU) ikilalamikia viwango vya malipo ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha vifurushi hadi kwa wenyewe kutokana na gharama kubwa ya uendeshaji, na kukataa kupokea vifurushi hivyo kama bei hazitaongezeka kufidia gharama za uendeshaji. Umoja wa Posta Duniani ulishughulikia suala hilo kwa haraka ili kuhakikisha kuwa umuhimu wa kutatua suala hilo unaenda sambamba na umuhimu wa kuwepo ushirikiano mzuri ndani ya Umoja huo.

Maamuzi hayo ya makubaliano wa viwango vipya vya malipo ya kusafirisha vifurishi ndani ya nchi wanachama 130, yalifikiwa siku ya pili ya Mkutano huo ambao ulikubaliana kukubali mapendekezo kutoka fungu V kati ya mapendekezo mengine yaliyofahamika kama A, B, C ambayo hayakukidhi maoni ya nchi nyingi wananchama wa UPU.

Kabla ya kufikia makubaliano ya viwango vipya vya malipo, Tanzania ilikuwa imependekeza viwango vilivyoko kwenye fungu V. Katika Taarifa yake kwa Baraza Kuu la UPU, Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania Dk. Jim Yonazi, aliupongeza Uongozi wa UPU kwa kuhakikisha kuwa makubaliano yanafikiwa na kupendekeza kwa wajumbe wa Mkutano huo kukubali viwango vipya vya malipo vilivyoko kwenye fungu V.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na wajumbe wa Mkutano huu kumshukuru Mwenyekiti wa Mkutano huu na Mkurugenzi Mkuu wa UPU kwa namna mnavyoendesha Mkutano huu muhimu. Napenda pia niwashukuru wajumbe wote wa nchi wanachama wa UPU ambao wanakubaliana na mapendekezo yaliyoko katika kifungu cha V. Huu ni ushindi wetu sote kwani tumejadiliana kwa umakini mkubwa na kufikia uamuzi ambao ni bora kwetu sote. Sisi Tanzania tunapendekeza na kuwaomba wote tukubaliane na mapendekezo haya.” Aliwasema Dkt. Jim Yonazi wakati akiwakilisha msimamo na mapendekezo ya Tanzania.

Akifunga mkutano huo, Katibu Mkuu wa UPU Balozi Bishar A. Hussein aliwapongeza wajumbe Zaidi ya 800 kutoka nchi wanachama 130 kwa kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu gharama mpya za kusafirisha vifurushi kwa nchin wananchama wa UPU.

Balozi Hussein aliuleza Mkutano huo kuwa ‘hakuna changamoto yeyote inaweza kutushinda kama tukiamua kufikia maelewano kwa faida ya nchi zetu’. Aliwashukuru wanachama wan chi wanachama wa UPU kwa kwa kutatua changamoto kubwa ambayo miezi kadhaa nyuma ilionekana kubwa na isiyo na ufumbuzi.

Nae Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ndio Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta la Uturuki, Kenan Bozgeyikaliushukuru uongozi wa UPU kwa kazi kubwa ya kuhakikisha Mkutano huo wa Dharura unafanyika na kufikia maamuzi kwa niaba ya nchi zote wanachama.

3 thoughts on “UPU Wakubaliana Malipo ya Gharama Mpya za Kusafirisha Vifurushi na Mizigo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama