Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Uongozi wa Mahakama Dodoma Wafanya Jitihada za Kupata Mahakama za Wilaya

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Bi. Maria Francis Itala ( wa pili kushoto) akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba kufuatilia upatikanaji wa majengo kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma akitoa maelekezo kwa Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya Kondoa Bi. Edna Edward Dushi juu ya kuanza zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo ambapo Mahakama ya Wilaya ya Kondoa inajengwa.

Muonekano wa Mahakama ya Wilaya ya Kondoa, ujenzi ukiendelea

Muonekano wa jengo linalotumika kwa sasa na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa ambayo inatoa huduma za kimahakama kwa Wilaya ya Kondoa na Chemba.

Nyumba iliyoombwa kwa ajili ya makazi ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Chemba

Muonekano wa nje wa jengo lililopendekezwa kwa ajili ya Mahakama ya Wilaya ya Chemba

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Chemba akionesha eneo la kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba ambalo linapakana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Hakimu Mkazi Mfawidhi (M) wakitoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kwenda kuona eneo lililopendekezwa kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya pamoja na kuoneshwa kiwanja cha Mahakama katika Wilaya hiyo.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail