Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

UN Women Yatoa Vishikwambi 200 kwa Ajili ya Sensa ya Watu na Makazi

Na Lilian Lundo – MAELEZO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea vishikwambi 200 kutoka ofisi ya UN WOMEN Tanzania kwa ajili ya zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Salum Kassim Ali amevipokea vishikwambi hivyo kwa niaba ya serikali, Julai 2, 2022, Ofisi za TAKWIMU zilizopo Jijini, Dar es Salaam.

“Tumepokea Vishikwambi 200 vyenye thamani ya dola za kimarekani 85,000 kutoka Ofisi ya UN WOMEN Tanzania. Vishikwambi hivi vitatumika kwa ajili ya kukusanya data katika zoezi la sensa ya watu na makazi Tanzania Bara na Zanzibar,” alifafanua Salum.

32 thoughts on “UN Women Yatoa Vishikwambi 200 kwa Ajili ya Sensa ya Watu na Makazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama