Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ulega Ataka Kumalizika kwa Migogoro na Chanjo Kufikishwa Vijijini

 

Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameusisitiza uongozi wa Mkoa wa Pwani kutumia mkakati wa uvunaji wa mifugo kama mkakati wa kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na kuondokana na tatizo la uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata nyama mkoani humo.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo alipokutana na uongozi wa mkoa huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, wakati akitoa taarifa ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Pwani na kufafanua kuwa ni vyema uongozi huo ukafanya tathmini ya kina kwa kuunda kamati maalum ili kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji mkoani humo.

Amesema viongozi ndani ya mikoa yote nchini ni vyema wakaunda kamati maalum za wataalamu kwenda wilayani hadi vijijini ili kutafuta ufumbuzi wa haraka na kudumu wa kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji, ukiwemo mkakati wa kuhakikisha wafugaji wanavuna mifugo yao kwa kuuza katika viwanda vya kuchakata nyama ili vipate malighafi na kuuza nyama ndani na nje ya nchi.

One thought on “Ulega Ataka Kumalizika kwa Migogoro na Chanjo Kufikishwa Vijijini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama