Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kwenye Mji wa Serikali, Ihumwa Dodoma Washika Kasi.


Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa Serikali, Ihumwa, linaloendelea kujengwa na Mkandarasi Mzinga Holding Company, tarehe 13 Januari, 2019, Dodoma.

Mmoja wa mafundi wa Mkandarasi Mzinga Holding Company, akijenga sehemu ya ukuta wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu, katika mji wa serikali, Ihumwa Dodoma, tarehe 13 Januari, 2019.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akikaribishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Nigel Msangi, alipofika kukagua shughuli za Mkandarasi Mzinga Holding Campony, anayejenga jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa serikali Ihumwa Dodoma., Mkandarasi huyo yupo chini ya Wizara ya Ulizi, mwingine ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA-JKT, Kanali Rajab Mabele, tarehe 13 Januari, 2019.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akipata maelezo kutoka kwa Mratibu Ujenzi jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mkandarasi Mzinga Holding Company, Kapteni, Erick Siara wakati alipofika kukagua shughuli za Mkandarasi huyo katika mji wa serikali, Ihumwa , Dodoma, Mkandarasi huyo yupo chini ya wizara ya Ulizi, tarehe 13 Januari, 2019.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail