Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ujenzi Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar -Moro wafikia asilimia 73

*Kipande cha Moro-Singida ujenzi wapamba moto*

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam mpaka Moro-
goro chenye urefu wa kilometa 205 umekamilika kwa zaidi ya asilimia 73 huku
utandikaji wa reli ukiwa umemalizika na kazi inayoendelea kwa sasa ni uwekaji
wa nguzo za umeme, nyaya pamoja na ujenzi wa vituo mbalimbali vya kuhudu-
mia abiria na mizigo.

Akizungumza na Maafisa kutoka Idara ya Habari – MAELEZO, waliofanya ziara

katika mradi huo, Meneja Msaidizi wa mradi wa SGR kipande cha Dar es Salaam
hadi Morogoro, Mhandisi Ayouba Mdachi alisema kuwa baada ya ukamilikaji wa
utandikaji reli, sasa vituo vinaendelea kujengwa ambapo hadi sasa tayari jumla
ya vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro viko hatua za mwisho kukami-
lika.
Aidha katika hatua nyingine kipengele cha pili cha ujenzi huu ni kutoka mkoa
wa Morogoro hadi Makutupora Singida ambacho kimekamilika kwa zaidi ya asi-
milia 26.

Kwa upande wake Meneja wa Ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha Morogoro
hadi Singida Makutupora, Mhandisi Faustine Kataraiya alisema “ujenzi huu una-
fanyika usiku na mchana na tayari mahandaki manne yamejengwa sehemu
mbalimbali zenye milima ambapo treni itapita na madaraja sehemu zenye
mito”.
Aidha, kati ya mahandaki manne yaliyojengwa Morogoro na Singida, handaki
lenye urefu kuliko yote linajengwa chini ya safu za milima ya Ukaguru ambalo
lina urefu wa kilometa 1.2, huku daraja kubwa likijengwa mto Mkondoa Moro-
goro ikiwa ni utatuzi wa kero ya mafuriko ambayo hupelekea kusimama kwa
shughuli za usafiri wa treni kwa kipindi cha msimu wa mvua nyingi kwa reli ya zamani.

288 thoughts on “Ujenzi Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar -Moro wafikia asilimia 73

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama