Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Uhamiaji Kuwasaka Wahamiaji Haramu Ngorongoro

Dkt. Makakala amesisitiza kufuatwa kwa sheria za nchi pale wageni wanapotaka kuingia au kutoka nchini, na kwamba Uhamiaji imejipanga vema kusimamia eneo hilo katika mipaka yote nchini.

“Nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ambayo yanavutia wahamiaji haramu kufika nchini kwa sababu tofauti, hatutakubali hilo litokee wakati wowote ule,” amesema Makakala.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwalimu Raymond Mangwala amemfahamisha Dkt.Makakala kuwa Wilaya yake inaendelea vema na utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo na kwamba atatoa ushirikiano katika zoezi la kusaka wahamiaji haramu ili wale wote watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.

61 thoughts on “Uhamiaji Kuwasaka Wahamiaji Haramu Ngorongoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama