Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tutumie Siku ya Eid kwa Kutenda Mema-Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waislamu wote nchini watumie siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane.

“Leo ni siku kubwa na muhimu waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Swala ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwari, Msasani jijini Dar es salaam

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwenu na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Msikiti wa Anwari uliopo Msasani jijini Dar es salaam, Sheikh Alhaji Suleiman Mohammed wakati alipowasili msikitini hapo kuswali Swala ya Eid El Fitr

“Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”

Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto baada ya kushiriki Ibada ya Eid El Fitr kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani jijini Dar es salaam

Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo.

Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.

 

17 thoughts on “Tutumie Siku ya Eid kwa Kutenda Mema-Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama