Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tumieni Diplomasia na Mawasiliano Kuitangaza Tanzania Dkt.Abbassi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbassi akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wanaochukua shahada ya Mawasiliano ya Umma leo jijini Dar es Salaam.

Na. Grace Semfuko

Wanadiplomasia na wanataaluma ya mawasiliano nchini, wametakiwa kuitangaza Tanzania katika mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwenye masuala ya amani,utulivu wa kisiasa na sera nzuri ili kuwavutia watalii na wawekezaji kuja nchini, hatua ambayo itakuza pato la Taifa.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, wakati akizungumza na wanachuo wa mwaka wa pili wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma wa Chuo cha Diplomasia, Jijini Dar es Salaam kwenye mjadala maalum kuhusu Mahusiano ya Umma na ya Kimataifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbassi akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wanaochukua shahada ya Mawasiliano ya Umma.

Dkt Abbasi alisema ni muhimu kwa wanataaluma wazalendo kuitangaza nchi yao kwa mazuri ili fursa pana za uwekezaji zilizopo kuwafikia wawekezaji na watalii kuitumia nafasi hiyo ambayo pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na nchi mbalimbali pia itaongeza imani kubwa kwa jamii za kimataifa.

“Ni muhimu kwa wanadiplomasia na Wanamawasiliano wetu wa Kitanzania tukaitangaza nchi yetu, Tanzania ni nchi ya amani,hata kama kuna wanaojaribu kuitangaza vibaya nchi yetu wataumbuka tu iwapo sisi wanataaluma tutasimama kidete kuitetea”,alisema Dkt Abbasi.

Kila Mtanzania ana wajibu wa kuiongelea vizuri Nchi yake, ukiona mtu anazunguka huko Duniani kuichafua nchi yake huyo hayuko sawa”,alimalizia Dkt Abbasi.

Dkt.Abbasi pia alizungumzia ukuaji wa uwekezaji nchini, ambapo alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli zaidi ya viwanda 3,000 vimefunguliwa na hivyo kuongeza pato la Taifa na ajira kwa watanzania.

Aidha aliwataka wanataaluma ya mawasiliano kwa umma kuwa kiunganishi kati ya taasisi na jamii katika kuzungumzia masuala ya kimaendeleo na akasisitiza kuepuka propaganda.

Dkt. Abbasi pia alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa Tanzania inaongoza kuwa na wawekezaji wengi hatua ambayo imetokana na kuwepo na sera nzuri za biashara na uwekezaji.

245 thoughts on “Tumieni Diplomasia na Mawasiliano Kuitangaza Tanzania Dkt.Abbassi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama