Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TRA Yaboresha Mfumo wa Mashine za EFD

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeboresha mfumo wa usimamizi wa mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD) kwa kuuwezesha kupokea taarifa zote za kila risiti inayotolewa na kuitunza katika seva zake ili kuwezesha nakala ya risiti hizo kuweza kupatikana wakati wowote inapohitajika.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Angelina Adam Malembeka, alietaka kujua mpango wa Serikali kuboresha stakabadhi za mashine za EFD ili zisifutike baada ya muda mfupi.

Mhe. Chande alisema kufutika kwa stakabadhi hizo baada ya muda mfupi kunasababishwa na matumizi ya karatasi zenye ubora hafifu na kubainisha kuwa karatasi zinazopaswa kutumika ni zile zenye ubora wa “thermal paper”.

17 thoughts on “TRA Yaboresha Mfumo wa Mashine za EFD

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama