Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TFRA Yawashauri Wakulima Kununua Mbolea kwa Pamoja

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kupitia vyama vya ushirika inawahamasisha wakulima nchini kununua mbolea kwa pamoja kutoka kwa wazalishaji/makampuni yanayoingiza mbolea moja kwa moja badala ya mkulima mmoja mmoja kununua kutoka kwa wafanyabiashara wa kati ili kununua mbolea hiyo kwa bei ya jumla  na hivyo kuipata kwa bei ya chini tofauti na kila mkulima akinunua kiasi kidogo cha mbolea.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ndani na ununuzi wa Mbolea wa Pamoja, Joseph Charos alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki.

Charos alieleza kuwa, kutokana na bei za mbolea katika soko la dunia kuendelea kuwa juu, bei za soko la ndani pia zimeendelea kupanda. alisema, kwa mfano, wastani wa bei ya mkulima (Retail price) kwa mbolea ya Urea umepanda kutoka Sh. 53,318 mwezi Desemba, 2020 na kufikia Sh. 104,069 mwezi Desemba, 2021 kwa mfuko wa kilo 50, wakati wastani wa bei ya mbolea ya DAP umepanda kutoka Sh. 66,995 mwezi Desemba, 2020 hadi Sh.  109,179 mwezi Desemba, 2021 kwa mfuko wa kilo 50 sawa na ongezeko la 95% na 63% mtawalia.

3 thoughts on “TFRA Yawashauri Wakulima Kununua Mbolea kwa Pamoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama