Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TCAA Yapata Dola Milioni Moja za Kudhibiti Usafiri wa Anga

Akizungumza katika hafla maalum ya uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema fedha hizo zitatumika kuboresha miundombinu ambayo kwa sasa inafanyika sambamba na maboresho yanayofanywa na Serikali katika Shirika la Ndege Nchini.

“Nawapongeza sana Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kazi nzuri ambayo mmeifanya mpaka kuwa miongoni mwa nchi chache ambazo zimepata fedha hizo, ni imani yangu kuwa hatutarudi nyuma hasa ukizingatia Serikali inaboresha Shirika letu la Ndege”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Naibu Waziri huyo ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha fedha zinasimamiwa vizuri ili kuleta tija na matokeo shahiki ili kubaki kwenye viwango vya juu vya usimamizi na udhibiti wa usafiri wa anga nchini.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Anga Duniani, Kanda ya Mashariki na Kati  (Estern and Southern African), Bw. Barry Kashambo, amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA jitihada mbalimbalimbali ambazo amekuwa akizifanya ambapo ndani ya miaka miwili ameipandisha asilimia za usalama na udhibiti  kutoka asilimia 50 na kufikia asilimia 67 na kufanikiwa kupata mkopo  kutoka katika Shirika hilo.

Kwa upande wake Mshauri wa Waziri kutoka Ubalozi wa China, Bw.  Xu Chen, amesema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Taifa.

Awali akitoa taarifa, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Hamza Johari, amesema fedha hizo zitaekelezwa kwenye mafunzo ya wataalam katika eneo la Usalama na  ununuzi wa vifaa mbalimbali ili kuimarisha udhibiti na kuongeza usalama katika usafiri huo.

13 thoughts on “TCAA Yapata Dola Milioni Moja za Kudhibiti Usafiri wa Anga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama