Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TCAA Yaongeza Ukusanyaji wa Mapato

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete, ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kupitia Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), ambapo katika mwaka huu wa fedha 2020/21 kimeweza kukusanya takribani Shilingi bilioni 2 kutoka Milioni 500 zilizokusanywa 2017/2018 na hivyo kuongeza mapato ya Mamlaka kufikia zaidi ya Bilioni 45 kwa mwaka.

Ameongeza kuwa makusanyo hayo yametokana na uwepo wa miundombinu bora ya chuo hicho kuwa ya kisasa ikiwemo mifumo ya kisasa ya mafunzo kwa vitendo (Simulator) za kufundishia kozi mbalimbali chuoni hapo.

Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Mamlaka hiyo na chuo hicho ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza TCAA kwa kuweka mikakati thabiti katika uthibiti katika usafiri wa anga na kuitaka mamlaka kuendelea kuwekeza katika wataalam ili kukidhi mahitaji ya udhibiti.

18 thoughts on “TCAA Yaongeza Ukusanyaji wa Mapato

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama