Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TBS Yazipiga Msasa Taasisi za Serikali katika Sekta ya Mazingira

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa semina kwa taasisi za
Serikali zinazojihusisha moja kwa moja na uondoshaji wa shehene na
mizigo bandarini kwa lengo la kulinda afya, usalama, mazingira, ulinzi
na ustawi kwa Watanzania.

Mafunzo hayo yamekuja baada ya kikao kilichofanyika Novemba 11 hadi 20
mwaka jana baada ya kuonekana baadhi ya taasisi za Serikali zilizopewa
jukumu la kuondoa shehena na mizigo bandarini zinachelewesha kazi hiyo
na kusababishia usumbufu na gharama kubwa kwa wateja.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa semina kwa
taasisi hizo za serikali, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Yusuf Ngenya
alisema semina hiyo inalenga kutoa elimu juu ya mifumo ya udhibiti wa
bidhaa zinazoingia nchini, usajili wa bidhaa zinazoingia nchini na
namna ya kufanya maombi kwa njia ya mtandao.

Dkt. Ngenya alisema miongoni mwa taasisi zilizoshiriki semina hiyo ni
pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Wakala wa
Huduma ya Ununuzi Serikali ni (GPSA).

“Lengo ni kuwapa fursa na kutilia mkazo suala la uondoshaji wa shehena
na mizigo bandarini,”alisema.

Alisema Shirika hilo lina majukumu manne ikiwemo kuweka na kusimamia
viwango vyote vya kitaifa, kutoa mafunzo na ushauri viwandani juu ya
uzalishaji wa bidhaa bora, kupima na kuhakiki vipimo vinavyotumika
viwandani na kuelimisha umma juu ya masuala yote yanayohusu uwekaji na
usimamiaji wa viwango na uthibiti wa ubora wa bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Athuman Kisumo, alisema
miongoni mwa mada zilizotolewa katika semina hiyo ni pamoja na usajili
wa bidhaa zinazoingia nchini,namna ya kufanya maombi kwa njia ya
mtandao na majadiliano juu ya changamoto za uondoshaji wa shehena za
mizigo bandarini.

35 thoughts on “TBS Yazipiga Msasa Taasisi za Serikali katika Sekta ya Mazingira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama